YAH: KUWATAKIA KHERI WANASUASO KWENYE MITIHANI
YA MWISHO WA MUHULA 1,3,5,7,9.
Ofisi ya Rais wa serikali ya wanafunzi SUASO inapenda kuwapongeza wanafunzi wote kufika mwisho wa muhula wa 1,3,5,7,9 kwani haikuwa kazi rahisi. Sambamba na pongezi hizo Ofisi ya Rais wa serikali ya wanafunzi inaomba wanafunzi kuzingatia mambo yafuatayo;
- Kukamilisha usajili wa kozi na kuchapa (print examticket) kabla ya kuingia kwenye mitihani. Hii ni kupunguza usumbufu wowote na kuwa na uhakika wa kumaliza usajili wa kozi.
- Kupitia sheria za mitihani nz kuzifuata ili kuepusha usumbufu wakati huu wa mitihani. Kwa kurahisisha bonyeza hapa Examination_regularities_and_Irregularities(1)[1]Ili kupata sheria za mitihani.
- Kuzingatia mavazi stahiki ambayo yanaruhusiwa ndani ya chuo na muonekano unaoruhusiwa kama inavyoelezwa kwenye sheria ndogo ndogo za wanafunzi (student bylaws) sehemu ya sita.
Zaidi Uongozi wa serikali ya wanafunzi kupitia Ofisi ya Rais unapenda kuwatakia wanafunzi wote kheri na mafanikio katika mitihani hii ya mwishoni mwa muhula wa 1,3,5,7,9.
IMETOLEWA NA
George J Temu
Katibu Mkuu Kiongozi SUASO