Mnamo tarehe 22/03/2018 ilifanyika semina ya ujasiriliamali mahali ni OASIS hotel Morogoro. Semina hio ililenga wadau mbali mbali wa shughuli za kiuchumi na maendeleo mkoani Morogoro. Semima hii ilikua ikiendeshwa Ubalozi wa India Tanzania kwa kushirikiana na Tanzania Chamber of Comerce and Agriculture (TCCA). Serikali ya wanafunzi SUASO ilipata mwaliko kupitia utawala wa chuo na kuwakilishwa na wanafunzi baadhi kutoka ndaki ya Kilimobiashara. Semina hio pia ilhudhuriwa na viongozi wa kutoka mkoani na wilayani pamoja na watu kutoka sekta mbali mbali za kiserekali na sekta binafsi. Aidha Semina hio ilijenga kuelezea mahusiano ya kibiashara kati ya India na Tanzania yaliyodumu kwa muda mrefu. Sambamba na Semina hiyo yalikuwepo maonesho mbali mbali ikiwemo madini, bajaji, pikipiki, solar power, madawa, vinyago na tractors. Semina hii ililenga kuongeza maarifa, tija, fursa na ufanisi Katika Biashara, Viwanda na Kilimo ili kujenga Tanzania ya Viwanda na Ubora wa hali ya juu. Kwa Maelezo zaidi tembelea
www.hcindiatz.org au morogoro@tccia.com.
http:/www.tccia.com
TAARIFA HII IMETOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU SUASO.